Sisi sote tunayo mahitaji
halisi. Makubwa kati ya hayo ni haya: upendo, usalama na umuhimu.
Ndani ya
mahitaji hayo, tunayo mahitaji mengine yaliyo wazi zaidi. Baadhi ya watu
wanahitaji chakula na mavazi, wengine wanahitaji watoto wao wamjue Mungu,
wengine wanahitaji kuponywa magonjwa, na mahitaji mengine kadha wa kadha.
Matumizi
ya mimea na matunda yanapunguza ukatili dhidi ya wanyama ambao kwa kiasi
kikubwa wamekuwa wakichinjwa kila siku kwa ajili ya vitoweo na wakati mwingine
wanyama hawa wametumika katika bidhaa mbalimbali.
Wanaotumia mimea na matunda wamejiepusha
kwa kiasi kikubwa na matumizi hayo kwa kwenda mbali zaidi kuacha kabisa kutumia
mazao mengine yanayotokana na wanyama na ndege hao kama vile nyama, mayai, na
asali pia matumizi ya ngozi.
Hata hivyo vegetarians wanaamini kuwa kuacha
kutumia vitu hivyo ni mojawapo ya njia ya kuwaokoa wanyama hao, pia kutunza
mazingira na kutunza afya zao wenyewe.
Tafiti mbalimbali za wanasayansi
zinaonyesha matumizi ya nyama ambayo ndani yake ina mafuta na protini ni chanzo
kikubwa cha magonjwa ya moyo, kansa ya mapafu na utumbo, kisukari, Unene wa
kupitiliza.
Hatuwezi kuziweka pembeni juhudi za Hom Jay Dinshah (1993-2000) ambaye
alipambana kusambaza elimu kuhusu matumizi ya mimea na matunda kipindi chote
cha uhai wake kupitia Jarida la Ahimsa (1960-2000).
Dinshah aliweka bayana
mchango wa wakongwe Mahtma Gandhi na Albert Schweitzer kama mhimili mkubwa wa
AHIMSA katika kitabu chake cha ‘Out of Jungle.’ Dinshah alizaliwa Novemba 2,
1933 na kufariki dunia Juni 8, 2000 akiwa na umri wa miaka 66 kwa mshtuko wa
moyo.
Imetayarishwa na Jabir
Johnson……………………….Oktoba 31, 2019
Tags
MASWALI NA MAJIBU