Mwinjilisti Genoveva Mikomanga, akionyesha kiapo. |
Makamu Mkuu wa Askofu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT), Dayosisi ya Mwanza Mchg Henry Kanyumi, amewataka Watumishi wa Mungu kuendelea kuimarisha amani ya nchi na siyo kuleta migogoro ndani ya makanisa.
Mchg Kanyumi aliyasema hayo Jumapili Novemba 11, 2019 wakati wa Ibada maalum ya kumweka wakfu na kusimikwa kazini, Mwinjilisti Genoveva Mikomanga, kuwa mtumishi katika Kanisa jipya la AICT Mlima wa Mizeituni katika ibada maalumu ambayo ilifanyika Makao Mkao Makuu ya (AICT) Makongoro Jijini Mwanza wengine waliowekwa wakfu na kusimikwa kazini ni Wazee sita wa kanisa hilo hafla ambayo iliyoongozwa na Makamu Askofu Mkuu wa kanisa hilo nchini.
Mchg Kanyumi alisema katika ulimwengu tuliopo sasa, migogoro imejaa na sasa inaonekana kama kitu chema na cha kawaida na migogoro hiyo inayoanzia katika familia, jumuia, vijiji, wilaya, mikoa na hata katika taifa letu kwa jumla.
“Ipo migogoro mingine baina ya ndugu na ndugu, jirani na jirani na hata pengine ya kabila na kabila, licha ya ile ya kimataifa, ipo pia migogoro ya kidini yaani kutokuelewana kati ya Mchungaji na Wazee wa kanisa, Mwinjilisti na wazee unakuta hawaelewani, madhehebu ya kidini na miongoni mwa waamini wenyewe kwa wenyewe na migogoro hiyo husababishwa na tamaa ya mali na madaraka, ubinafsi na chuki,”alisema Makamu Askofu Kanyumi.
Alisema hivi leo kuna familia ambazo haziwezi kukaa pamoja na kumaliza matatizo yao na badala yake huchukua njia za vita, ugomvi na hata pengine mauaji kama suluhisho la migogoro yao, na hiyo yote inatokana na familia hizo kutokuwa na nafasi ya kukaa pamoja na kuzungumza, watu wanaishi katika ulimwengu wa kuoneana mashaka na hivyo baadaye kuishia katika fujo.
Akizungumza mara baada ya kuwekwa wakfu Mwinjilisti Genoveva Mikomangwa, alisema anamshukuru Mungu hapa alipofika maana nilianza na kanisa lenye watu 55 hadi sasa ndani ya miezi mine ana zaidi ya waumini 400.
“Matarajio yangu ni kuona kanisa la Mungu linaongezeka, linakuwa na kukomaa, hata Bwana Yesu aliwahubiri watu 3,000 na waliweza kuokoka, hivyo natamani kuliona kanisa la Mungu, si tu ongozeko la wingi wa watu bali kuona kanisa la Mungu linakomaa, natamani sana kuendelea kuwafungua wengine waliofungwa katika utumishi wa Mungu alionipa natamani kusimama kama mtumishi Deborah, liko kusudi kwani dunia bado ipo gizani,”alisema Mwinjilisti Mikomangwa.
CHANZO: JAIZMELA NEWS
Tags
TANZANIA