Ni
Jumatano jioni, Rachel mwenye umri wa miaka 17, amemaliza kazi zake za nyumbani
naye anataka kupumzika!
Anawasha
runinga na kuketi kwenye kiti anachopenda.
Wakati
huohuo, mama yake anaingia, naye hana furaha.
“Rachel!
Kwanini unapoteza wakati ukitazama runinga badala ya kumsaidia dada yako
kufanya kazi za shule? Hufanyi kamwe unachoambiwa!”
“Umeanza
tena,” Rachel asema kimyakimya Mama akamkaribia,
“Unasema nini?”
“Hakuna,”
Rachel anasema akishusha pumzi, akizungusha macho kwa dhihaka.
Sasa
mama amekasirika kwelikweli. “Hutazungumza name kwa njia hiyo!”
“Na
wewe je?” Rachel amjibu.
Mapumziko
kwisha...ubishi mwingine umeanza.
Rachel anaongeza kuni kwenye moto kwa njia tatu, unaweza
kutambua njia hizo? Umewahi kujionea kisa kama hicho? Je wew na wazazi wako
mnabishana kila wakati. Ikiwa ndivyo, nini chanzo na suluhisho la changamoto
hiyo?
Tags
MASWALI NA MAJIBU