Na Johnson Jabir
MBEYA, TANZANIA
Hebu nikueleze mambo makuu zaidi. “Tunahesabiwa haki bure kwa neema yake” (Warumi 3:24).
Katika mahakama jambo kama hilo haliwezekani kabisa kwa mshitakiwa Hebu fikiria mfano wa mahakama na waamuzi wake, askari , kiongozi wa mashtaka, na hakimu. Waamuzi wamempata mshitakiwa kuwa na hatia. Mshtakiwa anasimama kitunduni akiwa amehukumiwa. Baadaye mahakama inatangaza kuwa mshtakiwa amekosa na lazima aadhibiwe na kulipa gharama. Kama angaliomba kufanya haki, mahakama nzima ingalimcheka pasipo kwamini ombi la mshitakiwa.
Watu wanapotaka kuwa na hakika, wengi wanategemea wanavyo jisikia. Hili ni kosa ambalo madhara yake yanaweza kuwa makubwa. Mungu hakusema kamwe kuwa kipimo cha wokovu wetu ni tunavyo jisikia. Ukweli hautegemei nafsi zetu bali neon lake Mungu.
Ingawa nafsi ya mwanadamu ni kiumbe cha Mungu iliundwa kugeuka kulingana na hali ya maisha, mara juu mara chin, furaha au huzuni,inalingana na mawazo yetu. HATA BAADA YA KUOKOKA.
Watu waliookoka hahana nyuso za kutabasam wakati wote kana kwamba wao ni vinyago vya mpira, lakini wameingia katika mpango asili wa Mungu kwa maisha yao na hawana haja ya kutumia hisi zao kama kipimo cha wokovu.
Kwa hivyo wokovu umesimamajuu ya mwamba wa milele. Yesu alisema, “Mbingu na nchi zitapita lakini maneno yangu hayatapita kamwe” (Mathayo 24:35).
Huu ndio ufa kwenye mwamba wenye imra ambapo inatupasa kukimbilia wakati wowote shetani anapotushambulia na mashaka.Nimeokoka kwa kuwa neon la Mungu linasema hivyo.Haidhuru ninavyojisikia, imani yangu bado ni imara.
Wakristo wa kwanza hawakuwa na mashaka kuhusu jambo hilo.Tunasoma kwenye maandiko ya kwamba “Walijawa na tumaini; wakiwa na furaha tele na neema kwa wingi”. Wingi unamaanisha vitu vya kutosha na zaidi, vingi zaidi kama vikapu kumi na viwilivya chakula vilivyosalia Yesu alipo walisha watu. Hakikisho la wokovu si tu kuwa na matumaini makubwa lakini ni amani shwari inayojaa ndani ya nafsi yako wakati shetani anapokunong’oneza maneno ya mashaka.
Paulo anawaeleza wakristo wa Kolosai kuwa wenye “utajili wote wa kufahamu wa uhakika” (Wakolosai 2:2). Neno hilo “utajiri” katika biblia ya kiyunani ni “ploutos” maana yake ni mtu anayetawala kwa ajili ya mali yake.
Ninatamani kuwa MWINGI KATIKA IMANI NDANI YA MUNGU. Katika waraka wa waebrania 6:11 na 10:22 twasoma juu ya hakikisho kamili na wathesalonike walikuwa na hakikisho kamili katika kweli . Hiyo ni kujazwa na kweli na kuwa mwingi wa imani katika Mungu.
NENO LA MSALABA
Mtume Paulo alipousubiri Kalintho alikuwa na udhaifu katika mwili wake. Hata alizungumza juu ya kukata tamaa ya kuishi. Mahubiri yake yalikuwa rahisi ya kueleweka na yalilenga moja kwa moja. Hakutumia nguvu au maneno ya kuwavutia waliomsikiliza, bali alihbiri “kwa dalili ya roho na ya nguvu” (1wakolintho 2:4).
Matokeo yake yalikuwa makubwa; wengi walitubu na kupokea wokovu. Hayo yaliwezekanaje? Kwani alihubiri nini hadi apate matokeo makubwa kama hayo? Mwenyewe alisema; “Maana naliazimu nisijejua neon lolote kwenu ila Yesu kristo, naye amesurubiwa” (Wakolintho 2;2)
Injili
MBEYA, TANZANIA
SHETANI HANA USHAHIDI
Hebu nikueleze mambo makuu zaidi. “Tunahesabiwa haki bure kwa neema yake” (Warumi 3:24).
Katika mahakama jambo kama hilo haliwezekani kabisa kwa mshitakiwa Hebu fikiria mfano wa mahakama na waamuzi wake, askari , kiongozi wa mashtaka, na hakimu. Waamuzi wamempata mshitakiwa kuwa na hatia. Mshtakiwa anasimama kitunduni akiwa amehukumiwa. Baadaye mahakama inatangaza kuwa mshtakiwa amekosa na lazima aadhibiwe na kulipa gharama. Kama angaliomba kufanya haki, mahakama nzima ingalimcheka pasipo kwamini ombi la mshitakiwa.
SHAHIDI WA KWANZA,
NENO LA MUNGUWatu wanapotaka kuwa na hakika, wengi wanategemea wanavyo jisikia. Hili ni kosa ambalo madhara yake yanaweza kuwa makubwa. Mungu hakusema kamwe kuwa kipimo cha wokovu wetu ni tunavyo jisikia. Ukweli hautegemei nafsi zetu bali neon lake Mungu.