WAONGOFU wapya wametakiwa kujazwa Roho Mtakatifu ili awasaidie katika Maisha yao ya Wokovu.
Akifundisha katika Darasa hilo Mwalimu na Mzee Patrick Nkwama alisema ili waweze kujazwa Roho Mtakatifu ni lazima waishi maisha ya kumpendeza Mungu kwa maana Mungu hawezi kukaa mahali pachafu. Mwalimu Nkwama alisema Roho Mtakatifu aliletwa kwa wale wote waliompokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa Maisha yao . Hata hivyo alitaja ishara ya kwanza kujua kuwa mwamini amejazwa Roho Mtakatifu kuwa ni kunena kwa lugha.