WAKRISTO
wametakiwa kujua kwamba matatizo makubwa katika serikali ya Tanzania yanatokana
na wao kutokuwa waaminifu mbele za Mungu katika kufanya Ibada ya Utoaji.
Akihubiri katika Ibada
ya Jumapili Mchungaji na Mwalimu Vinac Amnon Mwakitalu wa Kanisa la Tanzania
Assemblies of God Ilomba Christian Centre Mbeya amesema serikali nyingi
ulimwenguni ikiwemo Tanzania zimejikuta katika changamoto mbalimbali kutokana
na kanisa kutokuwa waamini katika utoaji wa mafungu ya 10 na sadaka mbalimbali.
Mchungaji Mwakitalu ameongeza kusema Mungu ndiye anayejua kipimo halisi cha
utoaji kwa mtu wa Mungu na kwamba kwa kufanya hivyo hakuna nayeweza kumdanganya
Mungu. Pia Mchungaji Mwakitalu amesema wengi wamefikiri kuwa kufunga na kuomba
sana ndio miujiza itafanyika huku wakisahau utoaji wa Mafungu ya 10 na sadaka
mbalimbali. Aidha Mchungaji Mwakitalu amebainisha Baraka za mwamini anayekuwa
mwamini katika utoaji wa sadaka na mafungu ya 10 kuwa Mungu atafungua madirisha
ya mbinguni na Baraka zake zitamiminika kwa mja wake.