Wito
umetolewa kwa viongozi wa nchi ya Tanzania kujiepusha na vitendo vya rushwa ili
nchi iendelee kuwa na Amani na Utulivu.
Akihubiri katika Ibada ya
Jumapili Mchungaji Benjamini Bukuku wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God
Amani Cathedral Centre lililopo Soweto Mjini Moshi amesema watanzania wamekuwa
wakijidanganya kwamba nchi hii haijaendelea katika Nyanja mbalimbali.
Mchungaji Bukuku ameongeza
kusema nchi hii imeendelea kweli kweli katika Nyanja ya rushwa hali ambayo
inaweza kuitumbukiza katika machafuko makubwa na umwagaji wa damu.
Pia amesema kwamba vitendo vya
rushwa vinavyoendelea kwa sasa vinaongeza laana kwa kila jambo ambalo Tanzania
itataka kulifanya halitafanikiwa kwani Mwenyezi Mungu atakuwa ameondoa mkono
wake.
Hata hivyo amewataka viongozi
wanaosimamia vitengo mbalimbali kusimama kidete kukemea rushwa ama kwa kupokea
au kutoa kwa kufanya hivyo huruma za Mungu zitairudia nchi ya Tanzania.
Aidha amekemea unafiki wa
baadhi ya viongozi nchini kujifariji kuwa nchi hii ipo salama huku wakiendelea
kufanya vitendo viovu.