SEHEMU
YA 1
PRINCE MOBUTU SEKO
Ushuhuda huu aliutoa Jumapili
ya tarehe 20, 2013 mjini Moshi nchini Tanzania alipokuwa akianza semina ya siku
7 ya “NGUVU YA UFUFUO KATIKA NENO LA
MUNGU KWA AJILI YA MKRISTO KWA MWAKA 2013”.
Itakumbukwa kwamba Mchungaji
Benjamini Bukuku wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Amani Cathedral Centre
alimwalika katika semina hiyo muhimu.
Kwa ufupi tu Mtumishi wa Mungu Prince Mobutu ni miongoni mwa maelfu ya
watu hapa ulimwenguni walioamua kuyakabidhi maisha yao kwa Bwana Yesu pia ni
miongoni mwa watoto wa Aliyekuwa Rais wa Zaire wakati huo sasa ni Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo Joseph Mobutu Sese Seko Ngbendu wa Zabanga.
Prince Mobutu nilimnukuu
mwenyewe (Johnson Jabir)
Anaendelea kusema katika
mahubiri yake siku hiyo nikiwa nimekaa kiti cha mbele nikimwangalia kwa makini
jinsi ambavyo akisikitika kwa jinsi alivyomkosea Mungu kabla.
“ Hakika watu wa Mungu mara
zote wengi wamekuwa wakizoea kuwaona wahubiri wasio na hela yaani maskini
wakisambaza Neno la Mungu lakini leo mimi ni mtoto wa aliyekuwa tajiri wa dunia
hata sasa, mtoto wa Rais wa Zamani wa Zaire Mobutu Sese Seko ninaeleza kweli ya
Neno la Mungu…Haleluya”.
Mtayarishaji
na Msimulizi: JOHNSON JABIR, MOSHI-TANZANIA