ESTA BUKUKU ni mwimbaji wa nyimbo za Injili hapa
nchini Tanzania mwenye maskani yake Mjini Moshi.
Esta ni mkristo wa Madhehebu ya Kipentekoste,
Tanzania Assemblies of God.
Husali katika kanisa la TAG Amani Cathedral
Centre Soweto Moshi.
Hakika utapendas huduma yake akisisimama mbele ya
hadhira kumuimbia Bwana.
Kama ujuavyo muziki ukishindwa kufikisha ujumbe
basi hakuna chochote ambacho kitafanyika, kwani hata mtoto huanza na toni ya
muziki anapozaliwa akiashiria kwamba anapenda muziki.
Ni wachache sana wanaoweza kujiendeleza kimuziki
kutokana na kutokuwa makini kwa lugha nyepesi tunasema hawajitambui kuwa
wao ni kina nani
ESTA BUKUKU AMEJITAMBUA KUWA ANAWAJIBU KWA JAMII
INAYOMZUNGUKA KUWA ANATAKIWA KUITUMIKIA KWA NJIA YA UMBAJI WAKE IWEZE
KUBADILIKA KIMWILI, KIROHO NA KIAKILI