ENDAPO Tanzania haitatubu
mbele za Mungu kutokana na matendo yake machafu ipo hatarini kukumbwa na balaa
la vita imebainika.
Askofu
Emmanuel Lazaro wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (T.A.G )anayehutubia
mkutano mkubwa mjini Arusha amebashiri kuwa nchi moja ya jirani itaivamia na
kuitwanga Tanzania.
Askofu
huyo ameenda mbali zaidi na kuitaja nchi hiyo kuwa Rwanda na kudai kuwa TZ
haitaiweza Rwanda!
Askofu
Lazaro amesema kwa damu na nyama Tanzania inajiona kuwa ina nguvu za kutosha
kivita hasa ikizingatiwa miezi michache iliyopita imepeleka majeshi yake nchini
Congo lakini mbele za Mungu si chochote.