Wanandoa katika Jiji la California
waliozaliwa siku moja na kuoana siku moja miaka 75 iliyopita wamefariki dunia siku moja.
UKISTAAJABU YA MUSA, UTAYAONA YA FIRAUNI…
Kwa
mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Long Beach Press Telegram, Helen na Les Brown
walifariki Julai 16 na 17 mwaka huu wote wakiwa na umri wa miaka 94.
Zach Henderson,
Mmilikii wa Grosari moja ijulikanayo kwa jina la Ma N’Pa iliyopo Long Beach
alinukuriwa wakisema kuwa alikuwa akiwaona wapendanao hao kila siku iitwayo kwa
Mungu na kuuita uhusiano wao kuwa “ a Wonderful Blessing”.
Kwa mujibu
wa taarifa iliyotolewa na Press –Telegram imesema kuwa wote walizaliwa siku
moja yaani Desemba 31, 1918 na pia walianza kuwa pamoja mwaka 1937 katika
masomo ya sekondari.
Imejulikana
kwamba wanandoa hao walikuwa waamini wa Mashahidi wa Yehova (Jehova Witnesses)
waliobarikiwa kuwa na mtoto wao Les Brown Jr.
Henderson
anasema imani yao kwa Mwenyezi Mungu ndio iliyozidi kuimarisha ndoa yao hadi
kufikia hapo.
Mtoto
wao Les Brown Jr alinukuriwa akisema “Walikuwa pamoja kila siku kwa miaka 75,
hakika upenndo wao ulilandana”
Post Telegram
limeripoti kuwa Les Brown alikuwa akiumwa ugonjwa wa Parkison’s na mkewe Helen
Brown alikuwa akisumbuliwa Kansa ya tumbo hadi mauti yao yalipowakuta
"She
was completely cognitive," Henderson said, describing how he found Helen
Brown a few days before she died. "It seems like she was waiting for Les
to be comfortable and they were going to move on to something else with each
other."
Ibada
ya pamoja itafanyika siku ya Jumamosi mchana kwa ajili ya kuwakumbuka wanandoa
hao huko Long Beach, California.
CHANZO:
JAIZMELALEO/ABC NEWS/YAHOO NEWS