Sifa za mwenye upako

NA MCHUNGAJI FIDELIS KALINGA, T.A.G CHANIKA, DAR
Kanisa la Tanzania Assemblies of God-Goshen, Chanika jijini Dar es Salaam 
Leo napenda kuzungumzia kwa ufupi kwa watumishi wenzangu na wanaotamani kujua mtu mwenye upako yukoje.

Zipo sifa nyingi za mtu mwenye upako wa Roho Mtakatifu lakini miongoni mwa hizo ni hii ambayo ningependa nikushirikishe japo kidogo.

Ni mtu adimu sina maana kila wakati utamkosa hapana lakini sio mzururaji, ambaye yupo yupo tu kila ukimtaka waweza kumpata.

Mtu mwenye upako ni mtu adimu anapatikana kwa ratiba hana muda usio na kazi.

Mara nyingi Yesu alitafutwa na akaulizwa unakaa wapi, akina Zakayo ilibidi wapande juu ya mkuyu ilikuwa sio rahisi kumpata Yesu

Ukiona mtu anapatikana kila wakati ukipiga simu tu umempata ukienda kwake tu umempata hata huambiwi subiri, ukimwita tu kaja hata kama ni baa, ukimwambia nisindikize kule mnaenda hata bila maandalizi kaa ule anakula tena kila nyumba.

Akiambiwa njoo uhubiri kesho anakuja bila hata kuona itamgharimu kuharibu ratiba fulani nk,ujue huyo hana chochote nimefa ya utafiti wa mtu mwenye kitu cha kiMungu ni lazima atakuwa adimu tu na siyo kiburi hapana Upako hutufanya tuwe adimu wakati fulani.

Post a Comment

Previous Post Next Post