Mungu anataka Umjue

Ukitaka mtu akujue unaweza kufanya nini? Utamwambia jina lako, sivyo? Je, Mungu ana jina? Dini nyingi hujibu kwamba jina lake ni Mungu au Bwana. 

Lakini hayo sio majina yake binafsi. Hayo ni majina ya heshima kama vile Mfalme au Rais. Biblia inafundisha kwamba Mungu ana majina mengi ya heshima. 

Baadhi ya majina hayo ni Mungu na Bwana. Hata hivyo Biblia inatufundisha pia kwamba Mungu ana jina lake binafsi, yaani YEHOVA. 

Andiko la Zaburi 83:18 linasema hivi; "Wajue ya kuwa Wewe, uitwaye jina lako YEHOVA; Ndiwe peke yako Uliye juu, juu ya nchi yote." 

Kwa hiyo Yehova anataka ulijue jina lake na kulitumia. Tunaweza kusema kwamba anatumia Biblia kujitambulisha kwako. Mungu alijipa jina lenye maana. 

Jina lake, linamaanisha kwamba anaweza kutimiza ahadi yoyote anayotoa na kufanya jambo lolote analokusudia. Jina la Mungu ni la Pekee katika njia mbalimbali. Jinsi gani? 
Tuliona kwamba andiko la Zaburi 83:18 likimtaja Yehova. 

Pia andiko la Ufunuo wa Yohana 15:3; " Nao wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa Mungu, na wimbo wa Mwana-Kondoo, wakisema, ni makuu na ya ajabu, matendo yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi; Ni za haki, na za kweli, njia zako, Ee Mfalme wa mataifa."

Jina 'Mweza-Yote' linatufundisha kwamba Yehova ndiye mwenye nguvu zaidi kuliko wote. Nguvu zake hazina kifani; ni nyingi sana. 

Andiko la Zaburi 90:2; " Kabla hajazaliwa milima, wala hujaimba dunia. Na tangu milele hata milele ndiwe Mungu." 

Yehova ni wa pekee kwasababu yeye peke yake ndiye Muumba. Andiko la Ufunuo wa Yohana 4:11; "Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima  na uweza, kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwasababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa."

Written by: Jabir Johnson
Date: March 24, 2020

Post a Comment

0 Comments