Je, majaribu yatoka kwa Mungu?

 

Waumini wa kanisa la PAG, Chukwani-Zanzibar katika Ibada ya Oktoba 22, 2019

Majaribu ni moja ya mambo makubwa ambayo wana wa Mungu kikamilifu wanapitia ,yamkini wengine inaonekana wanashawishiwa sana kuliko wengine. Hakuna mtu hata mmoja ambaye hawezi kuzuia au kujiepusha asipatwe na majaribu, Adam, Lusifa na Yesu walijaribiwa.

Mungu ametufundisha kuuweka huu mgawanyo katika maisha yetu ya kila siku ya kusali. “usitutie majaribuni /vishawishi, lakini utuokoe kutoka dhambini”

Baadhi ya Mitume wakubwa walisumbuka sana kwa sababu walifikiri kushawishi au jaribu ni lazima liwe ovu/uovu au baya. Lakini kushawishiwa au kujaribiwa siyo dhambi, dhambi ni kukubali kishawishi au kishawishi kinaposhinda au akikubaliana nacho.

Ushindi katika kishawishi kimoja unaweza kukusaidia kushinda na vishawishi vingine.

Hatuwezi kuwazuia ndege kuruka au kupaa angani juu ya vichwa vyetu, lakini tunaweza kuwazuia ndege hawa kuweka makazi au viota vyao kwenye nywele zetu; hatuwezi kuzuia mawazo ya dhambi katika fikra zetu, lakini tunaweza kuyazuia mawazo au fikra za dhambi kuweka makazi kwenye ufahamu wetu na fikra zetu.

Mtu mmoja alimwuliza swali msichana mdogo kuwa anafanya nini majaribu au vishawishi vikija? Akajibu, “majaribu au vishawishi ni kama shetani abishaye hodi moyoni mwangu, na nikimwona shetani anabisha hodi, namwita Yesu aje afungue mlango” Shetani anaganda na kutoweka anopomwona mwenye nguvu na mamlaka ya ushindi pale msalabani.

Yakobo 1:12

Heri mtu astahimiliye majaribu …….., anakataa majaribu na kuwa mshindi kwa kupitia damu ya Yesu Kristo aliyoimwaga msalabani.

1 Korintho 10:13.,

“Jaribu halikuwapata ninyi isipokuwa lililokawaida ya wanadamu ila Mungu mwaminifu ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo, lakini pamoja na lile jalibu atafanya na mlango wa kutokea ili mweze kustahimili.

Waumini wa kanisa la PAG, Chukwani-Zanzibar katika Ibada ya Juni 2020.

 Chanzo cha majaribu ni nini?

1.1 Mungu huruhusu ;

Hayatoki kwa Mungu

Yakobo 1:13

Mtu ajaribiwapo asiseme, ninajaribiwa na Mungu, maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu., kwa mfano Ayubu, Mungu alimpa shetani ruhusa ya kumjaribu Ayubu, lakini kwa kiwango Fulani tu. Ambacho Mungu aliruhusu.

(Ayubu 1:12, 2-6)

Mwili- Yakobo1:14.,

Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kujidanganya.

Hii inaonekana katika nyanja kuu tatu;

1. Tamaa ya mwili., -1 Yohana 2:16

2. Tamaa ya macho., -1 Yohana 2:16

3. Kiburi cha maisha ., -1 Yohana 2:16

4 Marafiki waovu ., Mithali 1:10., “Mwanangu mwenye dhambi akikushawishi wewe usikubali”

5 Wakristo marafiki., Mathayo 16:22,23., “…….Nenda nyuma yangu shetani wewe……” Yesu alimwambia Petro.

CHANZO: Pentecostal Assemblies of God Zanzibar

Post a Comment

0 Comments