Theolojia: Bustani nzuri



Mwanzo 1:11-25; 2:8-9 Tazama dunia hii! Kila kitu ni kizuri sana! Tazama majani na miti, maua, wanyama wote. 

Unaweza kumjua tembo na samba hapa? Bustani nzuri hii ilitokea namna gani? Na tuone Mungu alivyotuwekea dunia tayari. Kwanza, Mungu aliumba majani mabichi yaifunike nchi. Alifanya namna zote za mimea na miti midogo. 

Mimea hiyo inapamba dunia. Zaidi ya hivyo, mimea mingi inatupa chakula kitamu sana. Tena Munualiumba samaki waongelee katika maji na ndege waruke katika anga. Aliumba mbwa na paka na farasi; wanyama wakubwa na wadogo. Ni wanyama gani wanaokaa karibu na nyumba yenu? 

Je si vizuri kufurahi kwa vile Mungu alitufanyia vyote hivyo? Halafu, Mungu alifanya sehemu moja ya dunia kuwa ya pekee sana. 

Aliita bustani ya Edeni. Ilikuwa nzuri sana. Kila kitu ndani kilikuwa kizuri. Mungu alitaka dunia nzima iwe kama bustani nzuri hii. Lakini tazama tena picha hii ya bustani. Je! Unajua kitu ambacho Mungu aliona hakipo? Tuone. Mwanzo 1:11-25; 2:8-9

Post a Comment

0 Comments