VIFAHAMU VITA VYA MKRISTO


Na Johnson Jabir

ILOMBA Christian Centre, MBEYA-TZ

Soma Ef.6:12

“Kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama bali juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.”

Mkristo lazima utambue ya kuwa wetu si wa dunia hii na katika ulimwengu wa roho ndiko ambako vita vikali vinafanyika, vita hivi ni vikali kuliko hata vya mataifa ya hapa duniani yanayopambana uso kwa uso.

Majeshi ya pepo wabaya ni viumbe wanaofanya mashambulizi ya uharibifu na uangamivu dhidi ya maisha ya binadamu na viumbe wengi walio hai
Kwa asili “majeshi ya pepo wabaya” sio binadamu kama sisi.

Hivyo ukishamjua adui ni vizuri ukazitambua silaha ulizonazo na uwezo wa silaha ulizonazo, kwa neema ya Mungu, maandiko yameanisha aina za silaha na jinsi ya kuzitumia wakati wa mapambano.

Soma 2kor.10:4-5

“ Maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uweza katika Mungu hata kuangusha ngome, tukiangusha mawazo na kila kitu kijiinuacho kinyume na Mungu, na tukiteka nyara kila fikra ipate kumtii Kristo.”

Silaha hizo zinapatikana katika kitabu cha Ef. 6:13-20

Post a Comment

Previous Post Next Post