WAKRISTO WATAKIWA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU


Mwalimu Mhagama amewataka wakristo katika Kanisa la Tanzania Assemblies of God Ilomba Mbeya kujitambua kuwa kujazwa na kujaa Roho Mtakatifu hufanya watu wengine wavutwe kwa Kristo.
Akifundisha katika Shule ya Uanafunzi alisema kuwa Roho Mtakatifu hubadilisha mwenendo wa Mwamini na kusababisha wengine wavutwe kwa Yesu. Aliongeza kusema kuwa Roho Mtakatifu aliye ndani ya Mkristo anataakiwa  kuwa chanzo cha wengine kumjua Mungu aliyezifanya Mbingu na Nchi. BHata hivyo aliwataka waamini hao kujua kuwa Roho Mtakatifu anapokuwepo humfanya Mkristo kuwa na ujasiri katika kufanya kazi ya Mungu. Aidha alihitimisha kwa kusema kuwa Roho Mtakatifu hudumisha upendo ndani ya Kanisa, ushirika miongoni mwa wakristo na Mungu.
Katika Ibada hiyo walihudhuria waamini akali 109.

Post a Comment

Previous Post Next Post