HUDUMA ya World Agape yenye makao makuu Jijini Dar es Salaam na Matawi nchi nzima imeanza leo kufanya Maombi ya Uachilio kwa Taifa la Tanzania ikiwa ni katika kusheherekea miaka 50 ya Uhuru.
Taarifa kutoka kwa Mchungaji Joram Chole wa Kanisa la Agape Life la Sae Jijini Mbeya imesema madhumuni ya kuendesha maombi hayo kwa kipindi cha siku tatu ni kufanya Shukrani na Maombi kwa Mungu kwa ajili ya watanzania ili wote waliofungwa na nguvu za giza, umaskini, magonjwa waachiliwe kutoka katika utumwa huo.
Taarifa hiyo imeongeza kusema maombi hayo yatafanyika kuanzia Desemba 2-4 mwaka huu kuanzia majira ya 9 alasiri hadi 12 jioni pia katika mikoa 14 nchini Tanzania yanafanyika.
Jijini Mbeya yanafanyika katika viwanja vya Ruanda Nzovwe ambapo Mtume Dr. Vernon Fernandes wa Huduma ya Agape atahuduma katika maombi hayo.
Imeandikwa na Jabir Johnson Desemba 2, 2011.