STAND UP, STAND UP FOR JESUS


MTETEENI YESU.
Stand up, Stand up for Jesus.
Tenzi No. 71 Nyimbo Standard NS No. 373.
Na, George Duffield 1818-1888.
 
Hadithi ya kutisha sana inamhusu mwanatenzi wa Ki-marekani. Mnamo mwaka 1858, muda mfupi tu baada ya kuhubiri katika missioni kubwa iliyofanikiwa sana huko Philadelphia, Mwinjilisti na mpinga udhalimu wa kila namna Dudley Atkins Tyng alitembelea ghala kwenye shamba lake. Akinyoosha mkono wake kushika sehemu fulani ya mashine ya kukobolea mahindi, mkono wa shati lake ulinasa kwenye meno ya mashine ile na kurarua mbali mkono wake.
 
Baada ya masaa kadhaa kupita alikujakugundulika akiwa anaogelea kwenye damu yake, ajali iliyomgharimu Roho yake. Katika nyakati zake za mwisho kabla ya mauti yake, Mwinjilisti Dudley Atkins Tyng aliteta na mmoja wa wasaidizi wake, George Duffield (1818-88) akimwambia maneno: "Waambie mteteeni Yesu." Ujumbe ambao aliukusudia kwa washarika wake.
 
Duffield alienda nyumbani akiwa amehuzunika sana moyoni kufuatia kifo cha kiongozi wake Mwinjilisti Dudley Atkins Tyng na kutunga Utenzi wa Rohoni kama kumbukumbu yake, ambao aliusoma kama sehemu ya mahubiri yake yaliyofuata. Ulichapishwa kwenye gazeti la Sunday school na muda mfupi baadaye ukashika kasi na umaarufu mkubwa sana, kwa kiasi kwamba uliimbwa na pande zote za mapigano kwenye uwanja wa vita wakati vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipozuka.
 
Katika England, MTETEENI YESU ulikuja kuwa kiungo maarufu katika huduma za shule za umma, ambapo lyriki zake [maneno yake] “Stand up! Stand up!” yalikuja kusikika yakitumika kama kusisitiza nidhamu na ukakamavu/gwaride/mchakamchaka kuashiria shule au chuo kiko imara. Maneno ya MTETEENI YESU yalikujatumika sana pia kwenye sanaa za mwanasanaa maarufu mwingereza Lindsay Anderson ambaye ni mzaliwa wa India kama maneno ya hekima na busara kubwa. Hakika ni utenzi uliopendeka sana hata leo.
 
Vokali [vocal] yake ilikujatengenezwa na GJ Webb ambaye aliita hiyo vokali Morning Light [mwanga wa asubuhi], akiughani kutoka kwa sauti ya ndege mdogo wa rangi ya kahawia mwenye tabia ya kuimba kila asubuhi ambaye anaitwa lark wa jamii ya/ au kundi la Alaudidae, mwanzoni baada ya kuupa vokali, MTETEENI YESU uliimbwa kwenye parlours [majumba makubwa ya biashara] e.g. kwenye ma-supermarkets, ma-hoteli makubwa, madukani, kwenye vituo vya usafiri wa umma, kwenye sehemu zingine za biashara kubwa kama kitumbuizo kwa wateja.
 
Nilichojifunza:
Kumbe MUNGU ametumia hata ndege kumuimbia?! Kweli wewe na mimi tukikataa kumuimbia MUNGU basi atainua hata mawe yatamwimbia. GJ Webb alitembelewa na Roho wa MUNGU kumuongoza atoe sauti/vocal toka kwa ndege ambaye pia ni zao la kazi ya mikono ya MUNGU na akafanikiwa kuja na vocal iliyotetemesha dunia. Kumbe viumbe hivi tuvionavyo vipo kwa makusudi maalum ya muumbaji wao. Sasa tumeona jinsi ambavyo ndege mdogo sana aitwaye lark alivyofanyika mwinjilisti kwa kuiimbia kanisa na dunia nzima. Kwa kanisa ndege huyu apaswa kuwa nyara ya kanisa ambayo haistahili kuwindwa popote duniani. Ningekuwa GJ Webb ningeweka nembo ya huyu ndege na Mwinjilisti Dudley Atkins Tyng na George Duffield kuwa kama alama ya umiliki wa MTEENI YESU…. MPENDWA INUKA TUMWIMBIE BWANA.

KWA HISANI YA BLOGU YA SAMSASALI

Post a Comment

0 Comments