VIJANA WATAKIWA KUWA NA NIDHAMU MBELE ZA MUNGU

VIJANA katika Kanisa la Mungu wametakiwa kuwa na nidhamu katika huduma mbele za Mungu ili waweze kutimiziwa ahadi tele alizowaahidi.
Akifundisha katika Darasa la Uanafunzi Jumapili hii Mwalimu Joshua Matagane wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Ilomba Jijini Mbeya amesema utumishi wenye manufaa mbele za Mungu ni ule wenye nidhamu ndani yake.


Mwalimu Matagane ameongeza nidhamu ya kijana katika huduma huleta utakatifu, pia huharakisha majibu ya maombi ya kijana husika.


Pia amesema nidhamu hii husababisha ujasiri kuongezeka mbele za Mungu na Mungu hufikia mahali pa kumheshimu mtu wake.


Mwalimu Matagane amenukuru maandiko ya Wagalatia 5:16-21 na kusema tabia za mwilini zilizotajwa haziwezi kumpata kijana ambaye maisha yake yamejawa na nidhamu na kuongeza kuwa nidhamu hiyo huanza na maandalio ya moyo wa mwamini huyu na kumshawishi Mungu afanye kitu.


Aidha amesisitiza vijana kuachana na unafiki wa siku hizi kusifiana makaburini.


IMEANDIKWA NA JOHNSON JABIR JANUARI 15, 2011


Post a Comment

0 Comments