KANISA
la Tanzania Assemblies of God Ilomba Christian Centre Mbeya lilifanya Ibada
iliyojawa na nguvu za Roho Mtakatifu ikifuatiwa na Meza ya Bwana (HOLY
COMMUNION).
MCHUNGAJI PETER LYAKURWA
Mhubiri wa Neno la Mungu alikuwa Mchungaji Peter
Lyakurwa kutoka Chuo cha Biblia Itende Jijini Mbeya ambaye alihuburi kwa kina
kuhusu ROHO MTAKATIFU na kazi zake na kuongeza kuwa miongoni mwa dhambi ambazo
mwamini hataweza kusamehewa ni kumkufuru Roho Mtakatifu.
Mchungaji Lyakurwa aliweka bayana kuhusu uwepo wa Yesu katika kila kazi
aifanyayo Roho Mtakatifu kwamba Yesu hulithibitisha Neno lake na kuongeza kuwa
ni haki ya kila mwamini kujazwa na Roho Mtakatifu.
MCHUNGAJI PETER LYAKURWA AKIHUBIRI KANISANI ILOMBA MBEYA KWA MCHUNGAJI VINAC AMNON MWAKITALU