ZAIDI
ya shilingi milioni 3 zimetolewa kama ahadi kwa ajili ya kufanikisha semina ya
Pasaka itakayojiri miezi michache ijayo katika Kanisa la Tanzania Assemblies of
God Ilomba Jijini Mbeya.
MWANAJEOLOJIA WA BONDE LA ZIWA NYASA WITGARD D. NKONDOLA
Changizo hilo limefanywa jana Jumapili katika Ibada maalum
kanisani hapo na Mtumishi wa Bwana Mwanajeolojia wa Bonde la Ziwa Nyasa Witgard
Daniel Nkondola.
Katika ibada hiyo maalum ya changizo ilitanguliwa na
utambulisho uliofanywa na Mchungaji wa Kanisa hilo Vinac Amnon Mwakitalu.
Nkondola aliweka bayana kuwa mwamini ili aweze kula sahani
moja na Yesu sharti awe Mtoaji na hakuna njia ya mkato katika hilo.
Aliongeza kusema kumjaribu Bwana Mungu ni kwa njia ya kutoa
na kwamba utoaji lazima ufanyike kwa uaminifu na utoaji mzuri ni ule unatoa
kitu kilicho bora.
Hata hivyo alisema waamini wa siku za leo wamekubali kutoa
lakini sio vyote wanavyoweza kutoa hasa inapofikia wakati wa kutoa fedha na mali
zao.
Semina ya Pasaka inatarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi
3,040,000/=
Imeandikwa
na Johnson Jabir, Mbeya