KANISA la Tanzania Assemblies of God Ilomba Christian Centre
Mbeya, Machi 4 mwaka huu limesheherekea Sikukuu ya Wanawake katika Kanisa hilo
kwa kumtunza Mchungaji Vinac Amnon Mwakitalu kiasi cha Shilingi za Kitanzania
2,182,000.
WANAWAKE WA KANISA LA TAG ILOMBA MBEYA WAKIFUNGUA SIKUKUU YAO KWA MAANDAMANO KANISANI HAPO
Blogu ya JAIZMELALEO ilikuwepo Kanisa hapo tangu mwanzo wa
shamrashamra hizo majira ya saa 2 asubuhi hadi saa 10 jioni.
Mgeni Mwalikwa wa Neno alikuwa Mchungaji Rozina Janga kutoka
Kanisa la TAG Mbalizi Mbeya Vijijini.
MADHABAHUNI ILOMBA MBEYA
MAMA MCHUNGAJI MARIA MWAKITALU AKITABASAMU WAKIINGIA KANISA HAPO
KABLA YA MAANDAMANO TAG ILOMBA ILIKUWA HIVI
KINA MAMA WAKIZUNGUMZA JAMBO KABLA YA KUANZA
WENGINE WALIKUWA NDANI WAKIIMBISHA KUWAPOKEA WENZAO WALIKUWA NJE
WALIANZIA KWENYE GETI LA KANISA HILO LILILOPO MASHARIKI YA JENGO LA KANISA
KWA FURAHA KUU WALIINGIA KUASHIMISHA SIKU YA WANAWAKE KATIKA KANISA LA TAG