Masia mwana wa Mungu, kama Wakristo wanavyomwita
anabakia kuwa mwalimu pekee anayenukuliwa kwa sasa kuliko mwalimu mwingine
yeyote. Mafundisho yake yanakataa kujiweka katika dini fulani zaidi sana
yakigusa moyo wa mwanadamu na kuleta
matokeo. Hakuna kama yeye.
KILA
mwaka wakati kama huu huibuka wimbi kubwa la watu wanaoamini katika nadharia na
wengine wanaomkashifu kwa kutumia njia mbalimbali kuhusu Yesu wa Nazareti (K.K 4
– B.K 30–33) aliyekufa msalabani kwa kile kinachoamini dhambi za wanadamu.
Wengi
wao hujitahidi kwa nguvu zote kutafuta wapi kuliko na mashimo kuhusu Yesu
Mnazorayo (Yesu wa Nazareti).
Unamfahamu
msanii wa Marekani Douglas Blanchard?
Douglas Blanchard ni nani?
Blanchard
hufundisha masomo ya sanaa ya kuchora katika Chuo cha Bronx Community kilichopo katika Chuo Kikuu cha New York.
Mkufunzi
huyu huchora michoro kuhusu Yesu ambayo ina mtazamo wa kishoga (watu wanaofanya
mapenzi ya jinsia moja).
Aidha
Blanchard hutumia uzoefu wake katika
fani hiyo akijikita kwenye historia, elimu ya zamani kuhusu visasili na matukio
ya sasa.
Alizaliwa
katika jimbo la Dallas nchini humo, alitunukiwa Shahada ya Sanaa ya Uchoraji
(BFA) na Chuo cha Kansas City mwaka 1981.
Pia
alitunukiwa uzamili katika sanaa na Chuko Kikuu cha Washington mjini St. Louis
mwaka 1986 na mwaka 1993 alitunukiwa MFA na Chuo cha Sanaa cha New York Academy.
Anamiliki
studio yake ya uchoraji mjini Manhattan ya chini upande wa Mashariki.
Aidha
alithibitishwa kuwa muumini wa Anglikana (Episcopal) katika ngazi ya Uaskofu mwaka
1982.
Blanchard
alijipambanua kuwa mtu asiye na habari na Mungu na wala hawezi kuzijua.
Mwaka
2004 alifanya uzinduzi wa makumbusho yake kuhusu sanaa ya ushoga na usagaji
jijini New York na mwaka 2007 alizindua katika mji wa Taos, New Mexico.
Haikutosha
katika uzinduzi huo Blanchard alifanikiwa kuiweka hewani michoro yake katika
‘collection’ moja iitwaayo ‘The Passion of Christ: A Gay Vision’ yaani Mateso
ya Kristo katika mtazamo wa kishoga.
Huyo
ndiye Douglas Blanchard.
Makusudi
ya makala haya ni kutaka kumweleza Yesu katika mtazamo wa asiyefungamana na
dini yoyote, kwa lugha rahisi dini nyingine zina mtazamo gani kuhusu Masia
huyo.
Mhadhiri
wa Chuo Kikuu cha Oxford, England katika somo ya Kihindi, Shaunaka Rishi Das
alikaririwa akisema,
“Ni
vigumu sana kwetu kumweka Yesu huyu mpendwa wa Mungu katika kundi la Mkristo au
Myahudi. Kwani alikuwa akizungumza kuhusu Baba yake tu na hakujiingiza katika
siasa, dini au utajiri. Huduma kwa Mungu yalikuwa ni maisha yake, mapenzi yake
na dini yake.”
Yesu
pekee anabaki kuwa anayezungumzwa na kunukuriwa kuliko mwalimu mwingine yeyote
hapa ulimwenguni.
Mafundisho
yake yamekuwa yakigusa moja kwa moja moyo wa binadamu, hii imesababisha kuwa
Yesu kuwa kipekee bila kuegemea upande wowote wa dini zote hapa duniani.
Mwandishi
wa habari wa karne ya 20 Gilbert K. Chesterton (1874-1936) aliegemea katika mtazamo
kwamba Yesu amekuwa akionyesha uwezo wake katika vipindi tofauti, mila na
desturi tofauti na dini tofauti.
G.K
Chesterton kama alivyokuwa akifahamika na wengi alienda mbali zaidi kwa kusema
wakati Yesu akija duniani aliukuta utumwa wa hali ya juu katika maisha ya
binadamu, lakini alijitahidi kuifanya dunia iamini kuwa ulimwengu unaweza
kuwapo bila utumwa.
Katika
makala haya tunajiuliza Yesu alikuwa wa dini gani?
Rish
Das anatuachia maswali mengi katika kipindi hiki cha Pasaka,” Je, Wahindu
wanaweza kumfuata Yesu? Je Wahindu wanaweza kumpenda Mungu kwa moyo na nafsi
zao? Je unapaswa kuwa Mkristo ili umfuate Yesu? Sasa nani ni wa Yesu?
Imetayarishwa na Jabir Johnson........Machi 27, 2016
Tags
FIMBO YA MUSA