Waumini kote
nchini wametakiwa kumpa Mungu nafasi kwanza katika kila jambo wanalotaka
kulifanya sanjari na kuomba katika Roha na kweli ili waweze kukua kiroho.
Akihubiri
katika semina ya siku tatu, iliyofanyika katika Kanisa la Enlightened Christian
Gathering Church Of Tanzania (ECG), yaani Kanisa la Mkusanyiko wa Wakristo
Walio Angaziwa (ECG), lililopo Rau mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, Mchungaji
Praise Isakumbuka, alisema wakristo wengi hawakui kiroho kwa sababu hawajui
faida za kuabudu
Mchungaji
Isakumbuka, alisema kusudi la Mungu kukuumba mwanadamu ni kuwa na ushirika
naye, Mungu anafanya kila kitu , lakini hawezi kujiabudu yeye mwenyewe, hivyo amemuumba mwanadamu ili aweze kumwabudu
yeye.
“Kuabudu ni
maisha ya uchaji , unaweza kujitengenezea maisha yako ya baadae ukiwa hapa
duniani,”alisema Mchungaji Isakumbuka.
Alisema kuna
watu wanapitia katika mambo mengi magumu hivyo ni vizuri kumwalika Mungu
kupitia maombi, maana kupitia umoja huo kuna nguvu ndani yake.
Katika
semina hiyo iliyokuwa imebeba ujumbe wa ‘Adui aliyejificha nyuma yetu,’ alisema
kuna watu katika maisha yetu tuko nao, lakini hawapo nasi, wanakuwa kama nyoka
katika maisha yetu, hawa ndio wanaotufanya tusiweze kufanikiwa katika maisha
yetu, wanatufanya tushindwe hata kupata
usingizi nyakati za usiku.
“Sio rahisi
kugundua watu hao kama roho wa Bwana hayupo ndani yako, inahitaji ufunuo ili
kuweza kuwatambua watu hao wabaya katika maisha yetu.
Semina ya
neon la Mungu iliyofanyika katika Kanisa la Mkusanyiko wa Wakristo
Walioangaziwa (ECG) lililopo Rau mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro, ambapo katika
semina hiyo wengi iliwafungua na kujazwa na roho mtakatifu .
Katika
semina hiyo ya siku tatu iliyoendeshwa na Mchungaji Praise Isakumbuka wa Kanisa la Mkusanyiko wa
Wakristo Walioangaziwa (ECG), tawi la Mbeya, ambapo katika mahubiri yake Baba
mmoja aliyekuwa amepata ajali hiyo akawa anatumia ukosi wa shingo (Neck Colla
baada ya kuombewa na mtumishi huyo,
alipona na kuondoa ile Neck Collar).
Pia habari
hii imetolewa katika Gazeti la Kikristo la kila wiki la Nyakati Toleo Na. 958,
Jumapili Aprili 7-13, 2019
Story by:
Kija Elias
Gazeti la Nyakati Toleo Na. 958; uk. 3 |
Tags
TANZANIA