Mchungaji Benjamin Bukuku wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God-Soweto, Moshi. |
Kanisa la Tanzania Assembles Of God (TAG), linatarajiwa
kuadhimisha maadhimisho ya kutimiza miaka 80, tangu
kuanzishwa kwake mwaka 1939 ambapo maadhimisho hayo yatafanyika Jimbo la TAG
Amani Soweto mjini Moshi mkoani Kilimanjaro Mei 26 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Askofu Mkuu wa kanisa
hilo, Jimbo la Kilimanjaro Magharibi ambaye pia ni Mchungaji Kiongozi wa kanisa
la Amani Soweto, Dkt Benjamin William Bukuku alisema katika maadhisho hayo ambayo
yatatanguliwa na matembezi ya amani yataanzia katika kanisala la International
Christian Cente (KICC) la mjini Moshi hadi Jimboni ambapo kanisa la
TAG lililopo maeneo ya Soweto mjini Moshi mkoani hapa.
Alisema katika maadhimisho hayo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mkuu wa mkoa
wa Kilimanjaro Dkt. Anna Elisha Mghwira, pamoja na mgeni maalumu
kutoka makao makuu ya TAG Jijini Dar es Salaam
Mchungaji Moses Magembe.
“Katika maadhimisho haya tutakuwa na shughuli mbalimbali za
kijamii ambazo zitafanyika, moja wapo ni upandaji wa miti kuzunguka
eneo letu la Jimbo, ambapo zoezi hilo litafanywa na Mkuu
wa mkoa wa Kilimanjaro kwa kushirikiana na waumini
wote,”alisema Askofu Dkt Bukuku.
Aidha Askofu Dkt Bukuku, alisema katika maadhimisho hayo
pia waumini wa kanisa hilo, watatembelea katika gereza Kuu la
Karanga, kwa ajili ya kutoa huduma za neno la Mungu pamoja na
kuwapatia misaada mbalimbali ya kijamii wafungwa walipo katika gereza hilo.
Hata hivyo Askofu Bukuku alisema kanisa linajivunia kutimiza miaka 80 ttoka
kuanzishwa kwake na kwamba litaendelea kuhamasisha amani, umoja na mshikamano
kwa kueneza injili kwa mataifa yote.
Maadhimisho hayo yatakwenda sanjari na hitimisho la mpango
mkakati wa miaka 10 ya mavuno ambayo kilele
chake kitafanyika Julai Mwaka huu Jijini Arusha.
Kanisa la Tanzania Assembles Of God (TAG), linatarajiwa
kuadhimisha maadhimisho ya kutimiza miaka 80, Mei 26
mwaka ya tangu kuanzishwa kwake mwaka 1939 ambapo maadhimisho hayo yatafanyika
Jimbo la TAG Amani Soweto mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Pia katika maadhimisho hayo yatakwenda sanjari na hitimisho la
mpango mkakati wa miaka 10 ya mavuno ambayo kilele
chake kitafanyika Julai Mwaka huu Jijini Arusha.
Hayo yamesemwa na Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Jimbo la Kilimanjaro
Magharibi ambaye pia ni Mchungaji Kiongozi wa kanisa la Amani Soweto, Dkt
Benjamin William Bukuku, wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake kuhusiana na maadhimisho hayo.
Askofu Dkt Bukuku alisema katika maadhisho hayo ambayo yatatanguliwa na
matembezi ya amani yataanzia katika kanisala la International Christian Cente
(KICC) la mjini Moshi hadi Jimboni ambapo kanisa la
TAG lililopo maeneo ya Soweto mjini Moshi mkoani hapa.
Alisema katika maadhimisho hayo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mkuu wa mkoa
wa Kilimanjaro Dkt Anna Elisha Mghwira, pamoja na mgeni maalumu
kutoka makao makuu ya TAG Jijini Dar es Salaam
Mchungaji Moses Magembe.
“Katika maadhimisho haya tutakuwa na shughuli mbalimbali za
kijamii ambazo zitafanyika, moja wapo ni upandaji wa miti kuzunguka
eneo letu la Jimbo, ambapo zoezi hilo litafanywa na Mkuu wa
mkoa wa Kilimanjaro kwa kushirikiana na waumini
wote,”alisema Askofu Dkt Bukuku.
Aidha Askofu Dkt Bukuku, alisema katika maadhimisho hayo
pia waumini wa kanisa hilo, watatembelea katika gereza Kuu la
Karanga, kwa ajili ya kutoa huduma za neno la Mungu pamoja na
kuwapatia misaada mbalimbali ya kijamii wafungwa walipo katika gereza hilo.
Hata hivyo Askofu Bukuku alisema kanisa linajivunia kutimiza miaka 80 ttoka
kuanzishwa kawake na kwamba litaendelea kuhamasisha amani, umoja na mshikamano
kwa kueneza injili kwa mataifa yote.
STORY BY: Kija Elias
0 Comments