Makamu Askofu Mkuu wa Kanisa la
Assembles Of God (TAG), Jimbo la Kilimanjaro Magharibi, Mchungaji
Allen Lekei amewataka wafungwa walioko magerezani kujiweka mikononi mwa
Mungu siku zote za maisha yao ili kuepukana na changamoto za kuwa mbali na
Mungu.
Askofu Lekei aliyasema hayo wakati walipotembelea
wafungwa katika gereza Kuu la Karanga la Moshi na ikiwa ni maadhimisho
ya kutimiza miaka 80 pamoja na mpango mkakati wa miaka 10 ya mavuno ya
(TAG), ambapo waliwalisha neno la Mungu pamoja na kutoa misaada mbalimbali ya
kijamii yenye thamani ya shilingi laki 7.
Mchungaji Allen Lekei, alisema liko tumaini kwa
Mungu kwa watu waliovunjika moyo, waliokata tamaa, kwani hapo sio mwisho, kwani
kukaa mbali na Mungu kuna changamoto nyingi.
Aliwaasa kwa kuwatia moyo kuwa maisha wanayoishi
kwa sasa yasiwafanye kukata tamaa, kwani ipo siku Mungu atawwaonea
huruma hata wahukumu kwa dhambi zako.
Aidha aliwatia moyo kwa kuwasihi kuwa toba ina nguvu,
ina marejesho kwa Mungu, hivyo aliwaomba waendelee kuvaa mavazi ya
wokovu, mavazi ya upendo.
Akitoa nenoo la shukurani kwa niaba ya wafungwa
wenzake Mnyampara Mkuu wa gereza la wanawake Karanga, Sofia Kingazi, aliwaomba
kuendelea kuja na kutoa neno la Mungu.
“Tunashukuru mno kwa kuja na kutuona, kubwa zaidi
tumefarijika sana na ujumbe wa neno la Mungu, hivyo tunaomba msiishie
kuja leo tu kwa ajili ya kutulisha neno la Kiroho,”alisema Kingazi.
Kwa upande wake Mkurugenzi mstaafu wa Wanawake
watumishi Wakristo (WWK) Tanzania ambaye pia ni Mchungaji Kanisa la (TAG ) Chekereni
Lidia Materu, alisema kama unapita kwenye kipindi kigumu Mungu
anasema usiogope.
“Mungu ametupa agizo la kuwaona watu
waliofungwa, wagonjwa yatima na watoto yatima, hivyo ni vizuri kuwaona watu
wenye uhitaji watu wakipatanishwa na Mungu watajisikia kumtumainia
Mungu kuliko kutumia akili zao kwa mambo ambayo hayatawezekana,”alisema
Mchungaji Materu.
Mchungaji Materu aliongeza kusema kuwa “Ikiwa
umeshindwa kuulinda moyo wako kwa sababu ya kuzidiwa na mambo magumu na
mabaya , usikate tamaa, bado tumaini lipo, wengi hudhani kwamba
upako wa Roho mtakatifu ni kwa ajili ya kuhubiri habari njema na kuombea
wagonjwa tu, lakini neno la Mungu linaonyesha wazi kwamba
kuna upako wa kuganga mioyo iliyovunjika,”alisema.
Tags
TANZANIA