Theolojia: Mungu anaanza kuumba vitu



Yer. 10:12; Wakolosai 1:15-17; Mwanzo 1:1-10
Vitu vizuri vyote tulivyo navyo vimetoka kwa Mungu. Aliumba jua litupe mwangaza mchana, mwezi na nyota usiku. 

Tena Mungu akaumba dunia tukae ndani yake. Lakini kwanza Mungu hakuumba jua, mwezi, nyota na dunia. Unajua alivyoumba kwanza? 

Mungu aliumba watu walio kama yeye. Biblia inawaita watu hao malaika. Mungu aliumba malaika wakae na yeye mbinguni. Malaika mabaye Mungu aliumba kwanza alikuwa wa pekee sana. Alikuwa Mwana wa kwanza wa Mungu akafanya kazi pamoja na Baba yake. Alimsaidia Mungu kuumba vitu vingine vyote. 

Tena alimsaidia Mungu kuumba jua, mwezi, nyota, na dunia yetu. Wakati huo dunia ilikuwa namna gani? Mwanzoni mtu hangeweza kukaa duniani. Nchi yote ilikuwa bahai kubwa. Lakini Mungu alitaka watu wakae duniani. Akaanza kutayarisha makao yetu. Alifanya nini? Kwanza dunia ilitaka duru. Basi Mungu akaifanya nuru ya jua iangazie dunia. 

Alifanya hivyo ili kuwe usiku mchana. Kisha Mungu akatokeza nchi kavu juu ya maji ya bahari. Kwanza nchi haikuwa na kitu. 

Ilikuwa kama picha unayoona hapa. Maua hayakuwap, wala miti wala wanyama. Hata samaki hawakuwamo baharini. Mungu alikuwa na kazi zaidi ili dunia iwe makao yanayofaa sana ya wanyama na watu.

Mtayarishaji: Jabir Johnson


Post a Comment

Previous Post Next Post