Unawezaje Kustawisha Mazoea Mazuri?

Tuanze na mifano ya watu wawili 'Saa ya Austin inapopiga kengele ya kumwamsha, yeye bado huwa ana usingizi mwingi. Hata hivyo, huamka haraka, huvaa nguo za mazoezi alizotayarisha kabla ya kwenda kulala na kwenda kufanya mazoezi ambayo amekuwa akifanya tangu mwaka uliopita mara tatu kila wiki'.

'Laurie amegombana na mume wake. Akiwa amewaka hasira, Laurie anachukua mfuko uliojaa peremende (pipi) na kula peremende (pipi) zote, kama ilivyo kawaida yake anapokasirika.'
Austin na Laurie wana jambo gani linalofanana? Iwe wanajua au la, wote wanafanya mambo hayo kwasababu  wamezoea. 

Namna gani wewe? Je, kuna mazoea fulani mazuri ambayo ungependa kusitawisha maishani? Huenda umepanga kufanya mazoezi kwa ukawaida, kulala vizuri, au kuwa karibu na watu unawaopenda.

Kwa upande mwingine, huenda ungependa kuacha mazoea mabaya, kama vile kuvuta sigara, kula vyakula visivyo na lishe, au kutumia muda mwingi kwenye intaneti.

Ni wazi kwamba si rahisi  kuacha mazoea mabaya. Kwa kweli, wengine wamesema kwamba mazoea  mabaya ni kama kitanda chenye joto kali wakati wa baridi; ni rahisi kuingia lakini kutoka ni vigumu.
Hivyo unaweza kustawisha mazoea mazuri na kuacha mazoea mabaya? Chunguza mapendekezo matatu  yanayotegemea kanuni za Biblia.

1. Ona Mambo kihalisi

Sio kitu rahisi kubadili mara moja kila kitu ambacho umezoea kukifanya maishani mwako. 

Mithali 11:2 'Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu; Bali hekima hukaa na wanyenyekevu'.

mtu mnyenyekevu huwa ana siafa ya kuwa na kiasi, na mtu mwenye kiasi huona mambo kihalisi. Hutambua kuwa muda, nguvu na mali zake zina mipaka. 

Hivyo badala ya kujaribu kubadili kila kitu mara moja, atajitahidi kufanya maendeleo hatua kwa hatua. Haiwezekani kubadili mambo yote kwa mara moja au kwa wakati mmoja.

2. Chunguza Mazingira Yako

Azimia kuepuka mambo yasiyofaa na rahisisha mazingira ya kufanya mambo yanayofaa. Chagua marafiki kwa uangalifu. Tuna mwelekeo wa kuwaiga watu tunaoshirikiana nao. 

Kwa hiyo epuka kushirikiana na watu ambao watakushawishi urudie mazoea mabaya. Shirikiana na wale watakaokusaidia kustawisha mazoea mazuri. 

1 Wakorintho 15:33 'Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.'

3. Usikate Tamaa

Inaelezwa kuwa mtu anaweza kuzoea tabia mpya kwa siku 21. Hata hivyo utafiti unaonyesha kwamba huenda baadhi ya watu wakatumia muda mfupi  kuzoea jambo fulani ilhali wengine wakatumia muda mrefu.

Je hilo linapaswa kukuvunja moyo? Haijalishi tutashindwa mara ngapi lakini jambo la maana ni kufikia malengo.


Post a Comment

Previous Post Next Post