Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Evans Balama amelikemea
kampuni la Ununuzi wa Kahawa Wilayani Mbozi mkoani Mbeya (LIMA Ltd) kuacha
tabia ya kulitumia JINA LA YESU kulaghai wakulima wa zao hilo.
Akizungumza katika mkutano
wa Wadau siku chache zilizopita Balama alisema Uongozi wa Kampuni hilo umekuwa ukijifanya kumjua Mungu sana huku likiwaibia wananchi na wakulima wa
kahawa wilayani humo.
Balama aliongeza kusema
kulitumia Jina la Yesu visivyo ni kumuonea Yesu na ukuu aliokuwa nao kwani katika
huduma yake hakuwahi kumlaghai mtu yeyote katika Israeli na vitabu vingi
vinathibitisha ukuu na upekee wake.
Pia aliongeza kusema
Kampuni hilo
halitakiwa kutumia mwavuli wa dini kujinufaisha huku likijua ni kosa kisheria
kufanya hivyo.
Mbali ni hilo
aliweka bayana kuhusu kampuni hilo limekuwa
likinunua kahawa mbichi kinyume cha sheria ya zao hilo ya mwaka 2001 inayotaka kahawa inunuliwe
kwa kuzingatia madaraja yaliyopangwa katika sheria hiyo.
Balama aliongeza kusema
kahawa mbichi sio sahihi kabisa kununuliwa kwani inapunguza ubora wa zao hilo katika soka la dunia na kuwaacha wananchi na wakulima
wa zao hilo
katika hali ya umaskini.
Katika mkutano huo wa
wadau uliosimamiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Gabriel Kimolo huku mgeni rasmi
akiwa Profesa Jumanne Maghembe ambaye ni
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika hapa nchini.
Zao la kahawa kabla ya
mwaka 2007 lilikuwa chini nchini Tanzania lakini kwa sasa bei yake ipo juu
hivyo kuuza kahawa mbichi ni kumuone mkulima wa zao hilo na katika mmkoa wa
Mbeya Mashamba makubwa yapo Lunji, Utengule na Mpunguluma(Mbeya Vijijini),
Mbimba, Msumbi, Kanji Lalji, Shiwanda, Kamaro, Elton (Mbozi ) na mkoa Mbeya una
jumla ya hekta 156, 420 za zao hilo.