IBADA YA MAZIKO KATIKA BIBLIA

Usiku wa  Januari 18, 2012 majira ya saa 4 hivi blogu ya MCRCTV www.mcrctv.blogspot.com kwa ushirikiano na JAIZMELALEO www.jaizmelaleo.blogspot.com kulifanyika mahojiano na Meneja wa Redio Ushindi FM inayorusha matangazo yake kutoka Mbeya, Tanzania Mchungaji Matthew Sasali kuhusu : “Ibada ya Maziko” funeral ceremonies.



YAFUATAYO NI MAHOJIANO
JAIZMELALEO:
Biblia imeonyesha wapi utaratibu au kanuni ya kuzika mwili wa marehemu?
MCH. SASALI:
Ukweli ni kwamba Biblia imeelezea namna ambavyo watu wa jamaii ya Israeli walivyokuwa wakiwazika wapendwa wao kwenye mapango ya koo zao.
JAIZMELALEO:
Wewe kama Mtumishi wa Mungu ukitumwa kufanya kazi katika maeneo ambayo yanafanya Ibada ya maziko nje ya mila na desturi za jamii ya Israeli utafanya nini?
MCH. SASALI:
Hakuna kitu chenye mvuto  katika jamii yoyote ile kama “Ibada ya maziko” hivyo nikienda maeneo kama hayo ninachotakiwa ni kufanya utafiti  kujua kilicho nyuma ya ibada hizo.
JAIZMELALEO:
Je, kumzika mtu kwenye ardhi , kumchoma moto ana kuzika majivu yake kwenye mito, maziwa au bahari au aina nyingine ya ibada hiyo je ni ipi sahihi au halali au Biblia inasemaje?
MCH. SASALI:
Biblia haijasema ni utaratibu upi ni sahihi kufanya lakini nilivyoeleza hapo awali kuwa jambo la muhimu hapo ni kuangalia nyuma ya taratibu hizo Mungu Mwenyezi anatukuzwa. Katika mafunzo ya Elimu kuhusu Mungu (THEOLOGY) inataka mila na desturi zozote zile katika jamii husika inayopelekewa habari njema zikiwa na chembe chembe zilizo kinyume au hazimtukuzio Mungu zinatakiwa kuondolewa kwa gharama yoyote ile.
JAIZMELALEO:
 Hapa Afrika, na maeneo mengine barani Ulaya na Amerika;ibada ya maziko imekuwa ikifanyika kwa kuzika mwili wa mareehmu ndani ya ardhi na huku imani ya kikristo  ikizungumza “ uliumbwa kwa udongo… na utarudi kwa udongo…” wakati wa maziko. Je ni sahihi kibiblia?
MCH. SASALI:
Biblia “is very traditional” yaani yenye kukaa katika mila na desturi kuna mengi yamenadikwa humo na waandishi waliokuwa wa jamii ile ya kiisareli  wazaliwa wenye kufuata mila na desturi na kma ingeandikwa na waandishi wasiofuata tamaduni za Israeli nao pia ingekuwa hivyo hivyo ; cha msingi  hazikuwa zikienda kinyume na Mungu Mwenyezi, walikuwa wakizika kwenye mapango  ya koo na baadaye walikuwa wakihamisha mifupa ya marehemu wao na kuitunza. Kwa maeneo uliyoyataja hatuoni wakifanya hivyo…  
JAIZMELALEO:
Je tamaduni hizi; Hinduism, Buddhism, Confucianism, na Taonism unazizungumziaje katika Ibada za maziko za marehemu wao?
MCH. SASALI:
Cha kufanya ni kujua kilichopo nyuma ya tamaduni hizo ni kipi kama kuzika kwao wanapochoma miili ya marehemu wao hakuna athari katika imani ya kikristo hakuna shida. Kwani kuna wakati ukienda pupa kuzikomesha tamaduni hizo katika “funeral ceremonies” utaumbuka hata madhumuni ya Injili kuwakomboa kutoka huko hakutafanikiwa. Pia unatakiwa kujua unapoingia taratibu za maziko  nje ya jamii yao wataitafsiri  vipi kwani wanaweza kusema hizo ni mila za kizungu ambao wao hawzipendi; hali inayoweza kuhatarisha Injili kama itafanyika bila ya kufanya utafiti wa kutosha.
JAIZMELALEO:
Neno lako la Mwisho kwa watumishi wenzako wa Mungu kuhusu Kanisa na Injili kwa mataifa.
MCH. SASALI:
Watumishi wenzangu katika huduma hii  ya Injili  kwa mataifa wanatakiwa kuwa wavumilivu na wenye kufanya utafiti kwanza  kabla ya kluchukua uamuzi. Nina maana ya kwamba wapo watumishi baadhi yao ambao hufikiria mabadiliko yanaweza kutokea mara moja (abruptly) kitu ambacho sio sahihi. Kumtoa mtu kwenye kile alichokuwa akiamini  ni hatua ngumu ambayo inahitaji uvumilivu wa hali ya juu hasa kwenye zile tamadunio ambazo haziamini katika Kristo Yesu. Nahitimisha kwa kusema kuwa “MABADILIKO NI KAZI, NI HATUA”.

Post a Comment

Previous Post Next Post